Breaking News

KILA MWANAMKE


huzaliwa akiwa mzuri, hii ni zawadi ambayo kila mwanamke kabarikiwa nayo kutoka kwa Mungu.
:
Lakini urembo ni juhudi zako wewe mwanaume, ndiyo ni kazi ya mwanaume kuhakikisha mkewe anakua mrembo ili azidi kumvutia.
:
Nijambo la kila mwanaume kuhakikisha kuwa ule uzuri ambao mkewe kapewa na Mungu unaonekana.
:
Hapa sizungumzii mambo ya kujichubua, kujiongezea makalio au nini, hapana nazungumzia mwanamke kupendeza.
:
Ndiyo uhakikishe mkeo anakula vizuri ili awe na ngozi laini, anakuwa hana mawazo ili atabasamu kila mara na uzuri wake kuongezeka.
:
Kuhakikisha anavaa vizuri ili akuvutie. Wanawake wote unaowaona wamependeza na wanafuraha huko mitaani furaha zao hazikuja tu.
:
Wengi kuna mwanaumke kamili ambaye anahudumia na anahakikisha wanapendeza, sasa wewe ishia tu kutamani wake za watu wakati wakwako umemuacha humhudumii.
:
Nikuambie tu kama huwezi kuhudumia hata ukipewa huyo ambaye unamtamani leo huko mitaani utaishia kumchakaza tu na kumzeesha akaonekana si mzuri kumbe kakutana na wewe, 








Hakuna maoni