Breaking News

HAKUNA MWANAMKE MALAYA


   
:
Hakuna mwanamke malaya, wala hakuna mwanaume bwege! Mwanamke ambaye umekua ukimfukuzia kwa miezi 12 sasa ndiyo ametoka kulala na mwanaume ambaye wamekutana siku tatu tu zilizopita.
:
Mwanamke ambaye ulimtongoza na kumpata ndani ya wiki moja kuna jamaa mwaka wa pili sasa anafukuzia na ashaliwa pesa nyingi tu za kutosha wakati wewe hata hela ya bajaji hukutoa.
:
Kama ameona kitu kwako, akakupenda na kushindwa kujizuia ukampata kirahisi acha kupiga kelele na kusema yule binti ni MALAYA.
:
Lakini kwa wanawake, huyo jamaa ambaye mmekutana juzi tu lakini kashakununulia iPhone, hajawahi kumtumia X wake hata vocha.
:
Kama umebahatika akakupenda na kuchanganyikiwa kwa muda mfupi juu yako, acha kujidnaganya kwamba jamaa ni BWEGE ukaona hajitambui ni wa kuchuna tu!
:
Mwanamke akikupa mwili wake na kuchanganyikiwa juu yako haimaanishi kuwa ni MALAYA, hivyo hivyo mwanaume akiamua kukuheshimu na kukutunza haimaanishi kuwa ni BWEGE.








Hakuna maoni