Binaadamu una uwezo wa kupigwa mtihani mzito kiasi kila mtu akaamini huo ndio mwisho wako na hata wewe mwenyewe ukajikatia tamaa.
Lakini tusichokifahamu mara nyingine SIO kila mtihani unaokukuta wewe ni WAKO.. kuna muda WANAOPIMWA ni watu wa pembeni yako waliokuzunguka kutokana na YANAYOKUSIBU na si wewe, Mitihani yako ikawa njia ya kujua imani na roho zao ni ndogo ama kubwa kiasi gani juu yako. Kupitia mitihani yako utajua nani ni MTU na nani SI MTU KWAKO, hivyo hiyo ikawa kama njia ya kufumbuliwa macho na kujua atakaesimama na wewe, atakaeukimbia na hata atakaekutenga ama kukugeuka kwa yaliyokufika.
Na roho za ukweli za wanaokuzunguka ni ngumu kuziona ukiwa kwenye hali nzuri, ila zinajitokeza pale inapoonekana hakuna tumaini lolote la kuchomoka katika yanayokukabili, hivyo kila mwenye rangi yake atakuonesha kwa kipindi hiko!! Lakini ghafla hata wewe mwenyewe ukiwa hutegemei utashangaa MUNGU amekuchomoa kwenye mtihani wenyewe na kuwa shujaa wa moja kwa moja huku waliotegemea anguko lako wakibaki mdomo wazi na wewe ukiwa tayari UNAJUA wa ukweli ni nani na wa uongo ni nani.
Mara nyingine MITIHANI YETU ni njia za kuoneshwa watu wabaya na wema na hata kutenganishwa nao inapobidi maana huenda kwa maneno ya kawaida ikawa ngumu kujitenga nao mpaka litakapokukuta kubwa.
Hivyo jua sio kila mitihani inayotukuta sisi ni ya kwetu, sisi tunaibeba tu lakini WANAOPIMWA NI WENGINE, na matokeo ya kufeli na kufaulu yanabaki kwao kutokana na yanayotusibu.

Hakuna maoni